Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle cover logo

Mission Berlin 19 – Mahaba katika hali ya Vita Baridi

5m · Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle · 20 Mar 12:21

Zimesalia dakika 40 na Paul na Anna wanamkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu wanafika Berlin Magharibi. Lakini ni upande usioafiki. Mambo yanazidi kutatizika wakati Paul anapomwambia Anna kwamba anampenda. Anna anatakiwa kuwa Berlin Mashariki ili afanikiwe kutekeleza jukumu lake. Lakini amekwama upande wa magharibi. Kisha kuna tatizo jingine: Katika hali ngumu kama hiyo, Paul anamwambia Anna kuwa anampenda. Anamtaka Anna kuacha kutekeleza jukumu lake. Hata hivyo mchezaji anamwambia Anna kurudi mwaka 2006 ili aanzishe mpango mwingine. Dakika 35 zitatosha kupata suluhisho?

The episode Mission Berlin 19 – Mahaba katika hali ya Vita Baridi from the podcast Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle has a duration of 5:00. It was first published 20 Mar 12:21. The cover art and the content belong to their respective owners.

More episodes from Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Mission Berlin 26 – Jaribio la Wakati

Anna anapowasili mwaka 2006, anamwambia Paul inawabidi kuukwamisha mtambo. Lakini wanahitaji alama ya siri. Anna anaufuata muziki na mwanamke mwenye mavazi mekundu anawasili. Je atamzuia Anna kutimiza lengo lake? Anna amerejea mwaka 2006 na anamwonyesha Paul ufunguo wenye kutu unaonuiwa kukwamisha mtambo. Hata hivyo mtambo huo unahitaji alama ya siri. Anna anajaribu sauti za muziki DACHFEG. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kumtaka Anna kumpa ufunguo, lakini Anna anautia ufunguo kwenye mtambo na kisha kubonyeza alama ya siri. Je mwanamke mwenye mavazi mekundu atajaribu kuzuia kuharibiwa kwa mtambo? Au atabakia kuwa kumbukumbu, kama mtambo huo ulivyo?

Mission Berlin 25 – Vurugu

Muda unayoyoma na Anna anamuaga Paul kabla ya kurejea tarehe 9 Novemba mwaka 2006. Atakapowasili atakuwa amebakiwa na dakika tano pekee. Je zitatosha? Huku zikiwa zimesalia dakika chache Anna akamilishe jukumu lake, mchezaji anamshauri kutumia fursa ya zogo lililopo kuondoka pole pole. Lakini hataki kuondoka bila kumuaga Paul sawasawa. Anna anachunguza mchezo na kugundua anahitaji ufunguo uliochakaa kutekeleza jukumu lake. Anaitaji pia muziki. Je atarejea kwa wakati ufaao kutekeleza wajibu wake? Amesalia na dakika 5 pekee ili akamilishe vizuri jukumu lake.

Mission Berlin 24 – Saa inayopiga

Anna analipata kasha la chuma lililofichwa katika mwaka 1961 lakini hawezi kulifungua kwa kuwa limechakaa. Anapofanikiwa kulifungua anapata ufunguo wa zamani. Je huo ndio ufunguo wa ufumbuzi wa siri? Muda unayoyoma na Anna ni lazima afungue kasha la chuma. Lakini mchezaji anamtahadharisha kutolifungua mbele ya watu. Analifungua kasha hilo na kupata ufunguo wa zamani uliochakaa. Sasa anatakiwa kurudi mwaka 2006 ili akabiliane na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Lakini ana muda wa kutosha?

Mission Berlin 23 – Tutaonana baadaye

Anna anadandia skuta ili afike barabara ya Bernauer. Mhisani wake ni Emre Ogur anayemtakia ufanisi mjini Berlin. Lakini atahitaji nini zaidi kumkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu ili apate kasha la chuma lililofichwa? Mchezaji anamwambia Anna kutafuta usafiri wa kwenda barabara ya Bernauer kwa kuwa muda unamtupa mkono. Anadandia skuta inayoendeshwa na kijana mmoja, ambaye siku za usoni ni Inspekta Emre Ogur. Lakini Anna anapokutana na Heidrun Drei na Paul, mwanamke mwenye mavazi mekundu anawasili.Paul na Robert, mume wake Heidrun Drei, wanamrushia vipande vya ukuta. Wakati huo huo Anna anakimbia kwenda kuopoa kasha la chuma. Lakini je litakuwepo bado baada ya miaka yote hiyo?

Mission Berlin 22 – Endelea

Anna anapelekwa mwaka 1989 na anafika katika jiji ambalo lina kizaazaa cha kuanguka Ukuta. Anahitajika kupitia umati mkubwa wa watu ili apate kasha la chuma lililofichwa. Je atafanikiwa? Anna anapotaka kuondoka kuelekea mwaka 1989, waendesha pikipiki wanajitokeza. Mwanamke mwenye mavazi mekundu analiamuru kundi lake kumsaka Anna. Anamtaka Anna akiwa hai. Anna anaingia kwenye mtambo wa wakati na anarudi mjini Berlin mwaka 1989 wakati jiji hilo limezama kwenye shamrashamra za kuanguka ukuta. Lakini yuko katika lango la Brandenburg ambapo kila mtu anasherehekea. Anna anapaswa kwenda katika barabara ya Bernauer. Kwa dakika 30 zilizobaki, je anaweza kuharakisha kuuvuka umati wa mamilioni ya watu katika jiji hilo ambalo hapo awali lilikuwa limegawanyika?

Every Podcast » Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle » Mission Berlin 19 – Mahaba katika hali ya Vita Baridi