Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle cover logo

Tukio 21 – Papa katika Hamburg

13m · Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle · 25 Aug 23:15

Katika afisi ya Radio D hali ya joto imezidi mno. Paula na Philipp wanafurahi pale wanapopewa kazi ya kwenda pwani ambako papa ameonekana bandarini. Paula, Philipp na Ayhan wanatatizika kwa kiasi kikubwa. Joto limezidi afisini wala hawana kiyoyozi. Paula anatamani kwenda baharini, na Compu anamsaidia kufanya hivyo. Waandishi habari hao wanakwenda Hamburg kwasababu inasemekana papa ameonekana bandarini. Paula na Philipp wanashindwa kupita kutokana na umati wa watu ambao tayari wamefurika kwa nia ya kumwona samaki huyo mkubwa. Mambo pia si rahisi kwa mwalimu ambaye anashughulikia viambishi mwisho vya uhusika wa moja kwa moja wa vidhihirisho vya jinsia ya kiume. Neno la kukanusha "kein" linafuata mtindo sawa wa viambishi vya mwisho.

The episode Tukio 21 – Papa katika Hamburg from the podcast Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle has a duration of 13:25. It was first published 25 Aug 23:15. The cover art and the content belong to their respective owners.

More episodes from Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Tukio 26 – Kumuaga Ayhan

Hali ya huzuni imetanda katika afisi za Radio D. Ayhan anawaaga wenzake na anarudi nchini Uturuki. Ingawa wafanyikazi wenzake wamemwandalia hafla ya kumuaga, hawana la kuchangamkia. Paula anafika kazini asubuhi na kuwapata watu wote wakijitayarisha kwa sherehe. Hafurahii sherehe hizo kamwe: Ayhan anaondoka Radio D kurudi zake Uturuki kumsaidia baba yake. Katika harakati za kumuaga Ayhan, wafanyi kazi wenzake wameandaa hotuba fupi na zawadi ya kumbukumbu ya rafiki yake Eulalia. Kutokana na hafla hiyo ya kumuaga Ayhan, mwalimu hajishughulishi na sarufi. Hata hivyo anazungumzia maneno machache kuhusu nomino ambatani.

Tukio 25 – Kuzikaribisha Meli

Waandishi habari hao wanajitahidi kuelewa kauli "getürkt" na wanazuru bandari isiyo ya kawaida ambako kila meli hukaribishwa kwa namna ya kipekee.Katika Bandari ya Willkomm-Höft kila meli hukaribishwa kwa wimbo wa taifa la nchi inakotoka. Kwenye mchezo wao wa redio, Paula na Philipp wanachunguza asili ya mila hii-ambayo yumkini inahusiana na maana ya neno "getürkt." Wakati huo huo, Ayhan anatumia muda wake afisini kusoma vitabu kuhusu bundi. Kwa kuwa Eulalia hajui kusoma, Ayhan anamsomea. Tukio hili linashughulikia zaidi viambishi-awali vya vitenzi na jinsi ambavyo maana ya kitenzi hubadilika pale kiambishi-awali kinapobadilishwa.

Tukio 24 – Meza ya Mhariri

Bundi Eulalia anawasaidia Paula na Philipp kupata mwelekeo. Wanagundua kuwa wafanyikazi wenzao wa gazeti la Hamburg wanahusika kwenye ulaghai huo. Paula, Philipp na Eulalia wanagundua kuwa wafanyikazi wa gazeti la Hamburg walitunga njama yote ya kuweko papa katika bandari ili wapate kuuza nakala zaidi za gazeti. Baadaye, Philipp na Paula wanazozana kuhusu matumizi ya neno fulani. Philipp anatumai kwamba Paula atatulia pindi akimwalika katika Bandari ya Willkomm-Höft. Lau Philipp angezingatia zaidi maneno aliyotumia, Paula hangeudhika. Kiambishi-awali cha kitenzi kinaweza kuwa kifupi lakini kinaweza kubadilisha maana ya neno. Baadhi ya viambishi vya vitenzi hutenganishwa na kitenzi-jina.

Tukio 23 – Pezi la Papa

Paula na Philipp wanategua kitendawili cha mahali pa kwenda kumwangalia papa na kwa mara nyingine tena wanagundua ulaghai uliohusika. Hata hivyo mwanzoni sababu za tukio hilo si dhahiri moja kwa moja. Wakiwa katika harakati za kumtafuta mwanamichezo wa kuteleza baharini aliyetoweka, Paula na Philipp wanakutana na mpiga mbizi na hapo wanapata fununu. Mpiga mbizi alikuwa amewahangaisha nusu ya wakazi wa Hamburg kwa kujifunga pezi la papa mgongoni mwake. Wakati huo huo Eulalia amefika Hamburg tayari kusaidia. Pia naye amegundua kitu fulani. Eulalia amepata fununu ambayo huenda ikawasaidia Paula na Philipp- fursa nzuri ya kutumia wakati timilifu. Zingatia zaidi jinsi ya kutumia wakati uliopita hali ya kwendelea.

Tukio 22 – Mwanamichezo Aliyetoweka

Philipp na Paula wanafuata dalili za papa na kugundua jambo la kushangaza. Wanaingiwa na hamu zaidi wanapopata bao la kuteleza kwenye mawimbi ya bahari bila mwenyewe na pia makala ya gazeti inayowachanganya. Wanapoepukana na zogo la umati wa watu, waandishi habari hao wawili wanachunguza mahali papa alipopatikana. Wanapoona bao lililovunjika la kuteleza kwenye mawimbi ya bahari, wanaingiwa na wasiwasi. Kisha, kwenye gazeti moja la Hamburg wanaona picha ya papa—na wafanyikazi wenzao Laura na Paul ambao wanaonekana kuwa na wasiwasi. Lakini yote hayo yanahusiana vipi? Tukio hili linasisitiza viwakilishi-nafsi "sie" na "er," vinavyotumika pia kuelezea majina ya jinsia ya kike na ya kiume, ambavyo tayari vimezungumziwa.

Every Podcast » Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle » Tukio 21 – Papa katika Hamburg