Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle cover logo
RSS Feed Apple Podcasts Overcast Castro Pocket Casts
Swahili
Non-explicit
dw.com
5:00

We were unable to update this podcast for some time now. As a result, the information shown here might be outdated. If you are the owner of the podcast, you can validate that your RSS feed is available and correct.

It looks like this podcast has ended some time ago. This means that no new episodes have been added some time ago. If you're the host of this podcast, you can check whether your RSS file is reachable for podcast clients.

Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

by DW.COM | Deutsche Welle

Mission Europe ni somo la lugha lenye sehemu tatu: Mission Berlin, Misja Kraków na Mission Paris. Jitose kwenye bahari ya lugha ujifunze, Kijerumani.

Copyright: 2024 DW.COM, Deutsche Welle

Episodes

Mission Berlin 16 – Nimeuona mustakabali wako

5m · Published 20 Mar 11:32
Anna anaporudi nyuma hadi mwaka 1961, waendesha pikipiki wenye silaha bado wanamwandama. Mwanamke fulani asiyemjua anamwokoa. Kwa nini akafanya hivyo? Je Anna anaweza kumwamini? Genge la waendesha pikipiki linamwandama Anna. Anajificha kwenye duka la kuuza vyakula na wakati huo huo msimamizi wa duka anamwambia kwamba wakati wa kufunga duka umefika. Msaidizi wake anasema kuwa Anna ni rafiki yake. Keshia huyo anamchukua Anna hadi nyumbani kwake na anamwambia kwamba walisoma pamoja. Nyumbani kwake, keshia anamjulisha Anna kwa Paul Winkler, ambaye ni kaka yake.

Mission Berlin 15 – Abiria wa wakati

5m · Published 20 Mar 11:28
Katika Berlin iliyogawanyika, Anna anapaswa kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hilo silo tatizo la pekee. Ana muda wa dakika 55 kuchunguza lengo la RATAVA. Je ni ujenzi au kubomolewa ukuta? Mwaka 1961, Anna anajaribu kufika Kantstraße. Lakini Kantstraße iko Berlin Magharibi na yeye yuko Berlin Mashariki. Anna hawezi kwenda Magharibi kwa sababu serikali ya Ujerumani Mashariki imeanza kujenga ukuta. Baada ya kuanzishwa upya kwa mchezo, mchezaji na Anna wanagundua kuwa huenda malengo ni mawili: ujenzi au kubomolewa Ukuta wa Berlin. Wanabakiwa na dakika 55 kuchunguza kujua lengo la RATAVA.

Mission Berlin 14 – Kurejea siku za usoni

5m · Published 20 Mar 11:17
Anna anagundua mtambo wa wakati na anaambiwa kuwa genge la magaidi linataka kufuta tukio la kihistoria. Lakini tukio lipi? Mchezaji anamrejesha hadi mwaka 1961. Anasalia na dakika 60. Je amwamini mchungaji? Mchungaji anajua maana ya msemo "In der Teilung liegt die Lösung" na anaelewa hatari ya genge la RATAVA. Mchezaji anasema Anna anapaswa kurudi hadi mwaka 1961 ili kufumbua fumbo hilo. Mchezaji anaahidi atamrejesha Anna alikotoka pindi akifika mwaka huko. Mchungaji anampa msemo "Die Liebe versetzt Berge",…"Mapenzi husogeza milima"… ambao unamsaidia kurejea nyuma. Anaanzia tarehe 13 Agosti lakini akiwa na dakika sitini kutekeleza jukumu lake. Je muda huu unatosha?

Mission Berlin 13 – Msaada wa kichungaji

5m · Published 20 Mar 11:11
Kanisa linakuwa mahali pa kupata mwongozo. Mchungaji anamweleza Anna kuhusu sauti na kwamba sautii hiyo ni ufunguo wa mtambo wa wakati. Lakini anazungumzia kifaa gani? Mchezo unapoanzishwa tena, Anna na mwanamke mwenye mavazi mekundu wanagombana lakini mwanamke huyo anakimbia pindi mchungaji anapowasili. Anamwarifu Anna kwamba Inspekta Ogur amejeruhiwa na anajiuguza hospitalini. Mchungaji anaicheza tena sauti hiyo tena na kumwambia kwamba sauti za muziki D A C H F E G ndizo ufunguo wa mtambo huo. Ugunduzi huo unampa Anna na mchezaji dakika kumi za nyongeza. Lakini muda huo utatosha?

Mission Berlin 12 – Muziki wa Kanisa

5m · Published 20 Mar 11:07
Anna amebakiwa na dakika 65. Anatambua kuwa kikasha cha muziki ndicho sehemu inayokosekana kwenye kinanda cha kanisa. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kudai apewe ufunguo. Ufunguo gani? Anna anasikia wimbo anaoufahamu. Kinanda cha kanisa kinatoa mirindimo sawa na ile ya kwenye kikasha cha muziki. Wakati Anna anapokikaribia kinanda anamsikia mtunza kanisa akimweleza mgeni kuwa kinanda hicho kimerekebishwa ila kinakosa kipande kimoja…ein Element.. tangu ukuta ulipojengwa. Anna anatambua kuwa kikasha ndicho kiungo kinachokosekana na anakibandika kwenye kinanda. Kinanda kinapoanza kupiga, mlango unafunguliwa na anajikuta akiwa amekabiliana na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Anatokwa na uhai mwingine na anasaliwa na dakika 60 pekee.

Mission Berlin 11 – Mkahawani

5m · Published 20 Mar 11:02
Anna anamweleza Paul kuhusu msemo usioleweka, "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik!" Paul anatambua hatari iliyopo. Anamshauri Anna kumwendea Mchungaji Markus Kavalier. Je pendekezo lake ni sawa? Paul anatambua kuwa sauti iliyopo kwenye kikasha cha muziki haipigi mpaka mwisho wake. Kipande fulani kinakosekana. Anna anamwambia kuhusu ujumbe usioeleweka, "In der Teilun liegt die Lösung; folge der Musik!" Paul anampa "die Spieldose" na anamshauri kwenda kumwona Mchungaji Markus Kavalier katika kanisa la Gethsamane. Mchezaji anamwambia Anna kuwa mahali hapo palikuwa eneo la mikutano ya wapinzani wa utawala wa zamani wa Kikomunisti.

Mission Berlin 10 – Kizungumkuti

5m · Published 20 Mar 10:56
Mchezaji anazijumuisha tarehe 13 Agosti, 1961, siku ya kujengwa ukuta wa Berlin na tarehe 9 Novemba, 1989 wakati ukuta ulipoanguka. Mafanikio ya Anna kwenye jukumu lake yanategemea tarehe hizo. Anna afanye nini? Paul na Anna wanajificha katika duka kubwa la KaDeWe ambako Anna anacheza mchezo wake. Mchezaji anamwambia Anna kuwa ukuta wa Berlin ulijengwa tarehe 13 Agosti, 1961 na ukaanguka tarehe 9 Novemba, 1989. Anna atagundua kuwa ufumbuzi wa fumbo lote hilo ni kugawanywa kwa Berlin.

Mission Berlin 09 – Vidokezo vinavyokosekana

5m · Published 20 Mar 10:46
Anna anakimbia kutoka ukumbi wa maonyesho lakini mwanamke mwenye mavazi mekundu anamuwahi katika duka la Paul. Anna anafanikiwa tena kukimbia na kidokezo kimoja cha fumbo hilo na vipi apate kidokezo kingine? Ogur amemdokeza Anna kuhusu kundi la majambazi la RATAVA . Kwenye duka la saa, Paul Winkler anamwonyesha kwamba amekitengeneza kikasha chake cha muziki. Kinapiga wimbo uitwao "Nostagie" wa Friedrich August Dachfeg. "Ni wimbo wetu", Paul anamwambia Anna lakini Anna haelewi. Ghafla mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kufyatua risasi. Heidrun Drei anawasili na kupambana na mwanamke huyo ili kuwapa Paul na Anna fursa ya kukimbia. Anna amebakiwa na tarehe mbili: Agosti 13, 1961 na Novemba 9. Lakini mwaka gani?

Mission Berlin 08 – Kumaliza udhia

5m · Published 20 Mar 10:39
Ogur anamwarifu Anna kuhusu mpango muovu wa genge la RATAVA linalotaka kubadilisha historia. Kabla ya kupoteza fahamu, Inspekta Ogur anampa Anna tarehe. Novemba 9. Lakini mwaka gani? Ogur, anayeshuku kuwa Anna amejificha mahali fulani kwenye ukumbi, anamwagiza Anna kutoroka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anampiga Anna risasi na kumtoa uhai mara nyingine. Mchezo unaanzishwa tena na Ogur anamwambia Anna kuwa RATAVA ni kundi la majambazi wanaotaka kubadilisha historia. Ingawa Ogur amejeruhiwa, anampa kidokezo cha tarehe, Novemba 9. Lakini mwaka gani?

Mission Berlin 07 – Maadui wasiojulikana

5m · Published 20 Mar 10:33
Anna analikwepa genge la waendesha pikipiki na kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun, na Ogur anamwambia kuwa RATAVA wanamwandama. Lakini wanamtakia nini? Mchezaji anamwambia Anna kurejea dukani kwa Paul Winkler kuchukua kikasha chake cha muziki. Njiani inambidi kulikwepa genge la waendesha pikipiki kwa kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun Drei. Inspeka Ogur anawasili kumhoji Heidrun Drei kuhusu aliko Anna. Ogur anakisia kuwa Anna kajificha kwenye ukumbi huo na anamtahadharisha kwamba genge la RATAVA linamwandama. Wakati huo mwanamke aliyevalia mavazi mekundu anawasili.

Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle has 26 episodes in total of non- explicit content. Total playtime is 2:10:00. The language of the podcast is Swahili. This podcast has been added on November 27th 2022. It might contain more episodes than the ones shown here. It was last updated on February 8th, 2023 01:19.

More podcasts from DW.COM | Deutsche Welle

Every Podcast » Podcasts » Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle